Gharama
-
Ndani ya Wakati (siku 42):
Bei : 2500/= (Tzs)
-
Ndani ya Wakati (Miezi 3):
Bei : 7,000/= (Tzs)
-
Nje ya Wakati (siku 43 mpaka mwaka 1 na Miezi 11):
Bei : 22,000/= (Tzs)
-
Nje ya Wakati (Miaka 2 mpaka 5 na Miezi 11):
Bei : 32,000/= (Tzs)
-
Nje ya Wakati (Miaka 6 na kuendelea):
Bei : 42,000/= (Tzs)
-
Marekebisho:
Bei : 20,000/= (Tzs)
-
Kubadili Jina:
Bei : 30,000/= (Tzs)
-
Kufanya Upya:
Bei : 4000/= (Tzs)
Vizazi
Ni tukio la kizazi linalotokea nyumbani au hospitali ambalo linatakiwa lisajiliwe ndani ya siku 42.Tukio la kizazi linapotokea nyumbani muhusika anatakiwa kutoa taarifa kwa Sheha wa Shehia husika na kupata uthibitisho wa kizazi hai.
Utaratibu Ndani Ya Wakati:
- Kizazi hai (Tangazo la Kizazi)
- Kitambulisho cha baba na mama wa mtoto au cheti cha kuzaliwa cha baba au mama
- Gamba la cliniki la mama alilopimia wakati wa ujauzito.
- Cheti cha ndoa
Utaratibu Nje Ya Wakati (Baada ya Siku 42):
- Barua ya sheha wa shehia aliozaliwa Mtoto
- Kufika Wilayani kwa ajili ya kujaza Fomu ya Maombi