Gharama


Ndani ya Wakati (Miezi 3):

Bei : 1,500/= (Tzs)

Ndani ya Wakati (baada ya Miezi 3):

Bei : 3,500/= (Tzs)

Nje ya Wakati (siku 7 mpaka mwaka 1):

Bei : 11,000/= (Tzs)

Nje ya Wakati (Mwaka 1 mpaka Miaka 2):

Bei : 20,000/= (Tzs)

Nje ya Wakati (Miaka 2 na kuendelea):

Bei : 50,000/= (Tzs)

Marekebisho:

Bei : 20,000/= (Tzs)

Kubadili Jina:

Bei : 30,000/= (Tzs)

Kufanya Upya:

Bei : 4000/= (Tzs)

Vifo


Taarifa za Vifo zitapokelewa na Ofisa Usajili wa Wakala kutoka kwa Sheha. Sheha anatakiwa kupeleka taarifa kwa Mrajis ndani ya siku (7) za kifo kwa ajili ya kusajiliwa. Jukumu la kutoa taarifa za kifo ni la jamaa wa marehemu, aliyemuuguza hadi mwisho au mmiliki wa nyumba ambayo kifo kimetokea taarifa kwa Sheha wa shehia husika na kupatiwa kibali cha kifo

Wakala inasajili Vifo na kutoa Shahada Maalum (vyeti) vinavyothibitisha vifo hivyo)

Utaratibu Ndani Ya Wakati:
  • Kibali cha Mazishi
  • Kitambulisho cha marehemu ikiwa ana miaka 18 na zaidi
  • Kitambulisho cha aliekabidhiwa maiti
    • Mzanzibari Mkaazi
    • Mtanzania (NIDA)
    • Leseni ya Udereva
    • Hati ya Kusafiria
    • Kitambulisho cha Mpiga Kura
    Utaratibu Nje Ya Wakati:
    • Barua ya Sheha wa shehia kilipotokea Kifo
    • Hati ya kiapo
    • Kitambulisho cha alieapa
    • Kitambulisho cha Marehemu
    • Kitambulisho cha aliekabidhiwa maiti
      • Mzanzibari Mkaazi
      • Mtanzania (NIDA)
      • Leseni ya Udereva
      • Hati ya Kusafiria
      • Kitambulisho cha Mpiga Kura